Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal amesikitishwa na tuhumu ambazo ametoa mchezaji wake wa zamani wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria siku za hivi karibuni.

Mchezaji Angel Di Maria ambaye siku za hivi karibuni aliongea na vyombo vya habari na kueleza sababu mojawapo ya kuondoka kwenye klabu ya Manchester United kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na Mholanzi huyo.van gaalKocha huyo ambaye ndio alimsajili mchezaji huyo ndani ya Manchester United mwaka 2014 amesikitishwa na mchezaji wake huyo wa zamani kutokana na maneno hayo ambayo ameyazungumza, Lakini alionesha kutokujali kwasababu ana mahusiano mazuri na mchezaji wake wa zamani wa klabu hiyo pia Memphis Depay.

Van Gaal ameeleza Di Maria ni mchezaji mzuri sana wa mpira lakini kumtaja yeye kama kocha mbaya zaidi katika maisha yake ya soka ni sawa na kinyume chake kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji wachache sana ambao watazungumza hivo wakiulizwa juu yake.van gaalVan Gaal amesema Mchezaji huyo alikua anakumbwa na matatizo mengi ya nje ya uwanja jambo ambalo liliathiri utendaji wake wa kazi ndani ya kiwanja. Lakini kuna mchezaji kama Depay ambaye mpaka leo tuna mahusiano mazuri licha ya kua sikumpanga kwenye fainali ya michuano ya FA lakini hakununa.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa