Nyota wa Brazil na Real Madrid, Vinicius Jr, anaripotiwa kujaribu kuondoka kwenye mkataba wake wa Paundi Milioni 7 kwa mwaka na Nike baada ya kampuni hiyo kubwa ya nguo za michezo kumpa viatu vya zamani msimu uliopita.

 

Vinicius Jr

Vinicius Jr, 22, ambaye amekuwa mmoja wa taa zinazoangaza kwa nchi yake kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar, anahisi kutendewa isivyo haki na kampuni hiyo.

Kulingana na O Globo nchini Brazil, Vinicius Jr amewaambia mawakili wake kujaribu kumtoa kwenye mkataba wake na gwiji huyo wa mavazi ya michezo.

Kwa hali ilivyo, bado ana mkataba na anaendelea kuvaa viatu vya Nike kwenye Kombe la Dunia, ambapo alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 4-1 wa timu yake dhidi ya Korea Kusini Jumatatu jioni.

 

Vinicius Jr

Mkataba wa Vinicius Jr na mtengenezaji wa nguo za michezo utaendelea hadi 2028 na kesi hiyo iliwasilishwa kabla ya Kombe la Dunia.

Alivaa viatu vya zamani vya Nike Mercurial wakati Real Madrid ikikimbia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na mshambuliaji huyo mwenye kasi anadhani Nike inapaswa kumpa kutambuliwa zaidi kama mmoja wa nyota wao wakubwa.

Pia inasemekana hakuhudhuria hafla kadhaa za kampuni ya Nike.

Uchezaji wake akiwa na Real Madrid msimu uliopita na msimu huu umekuwa bora na kumpandisha kiwango kingine.

 

Vinicious Jr

Na mchezaji huyo wa zamani wa Flamengo ana mikataba na EA Sports, Vivo, Casas Bahia, BetNacional, OneFootball, JetEngage, Golden Concept na Royaltiz na Pepsi.

Ikiwa Vinicius Jr atafanikiwa kukata uhusiano na Nike, bila shaka kutakuwa na kinyang’anyiro cha kusainiwa kwake kutoka kwa washindani kama vile Adidas, Puma na Reebok.

Baadaye atakuwa kwenye kikosi cha Selecao watakapocheza na Croatia siku ya Ijumaa katika robo fainali ya Kombe la Dunia.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa