Maandalizi kuelekea mapambano ya WrestleMania yamepamba moto huku kukiwa na tetesi tofauti kuhusu baadhi ya mastaa wakubwa na ushiriki wao kwenye mapambano haya. Hapa nimekuletea tetesi za kuwahusu John Cena na The Undertaker, wakali wa WWE kulekea WrestleMania 35 April 7.
John Cena – WWE
John ena anaripotiwa kuwa BIZE na maandalizi ya movi yake mpya ya ‘Playing With Fire’ na muvi hii inadaiwa kuwa itakamilika hadi mwezi Aprili mwanzoni. Kwa maana hiyo ushiriki wa nyota huyu kwenye WrestleMania 35 ni wa mashaka kwa sababu ya ubize wake kwenye shughuli za filamu za Hollywood.
Kuhusu Undertaker
Huyu jamaa amekuwa ni mmoja wa kivutio kikubwa sana kwenye mapambano ya mieleka ya WrestleMania kwa kipindi cha miongo 3. Hata hivyo, nyota huyu mwenye miaka 54, amekuwa akipata majeraha mbalimbali kwa kipindi chote cha miaka yake ya kazi kwa miaka 29. Kuna taarifa kuwa nyota huyu hatashiriki WrestleMania 35.
Zeiyana
Undertaker big up