Yanga wapo sahihi sana kukubali kuvunja mkataba na Carlinhos Lakini kukubali kwao kuna sababu na moja ya sababu kwamba toka Carlinhos asajiliwe amewapa Yanga Muda mchache sana kiwanjani.

Mbili anaonekana hakuridhika na mazingira ya mpira wa Tanzania, Hakuwa tayari kucheza viwanja vya Tanzania, hasa Mikoani. Tunamlaumu nani kwenye Haya?

Yanga

Yanga wanapaswa kulaumiwa 100%. Na hili sio kwa Yanga tuu hata timu nyingine nyingi. Timu zetu zimekuwa na kawaida ya kufanya usajili bila kuwafwaatilia wachezaji, nina uhakika Yanga walimsajili Carlinhos bila kumfwatiliati zaidi.

Tunapozungumzia Scouting sio kumuangalia mchezaji anapocheza kiwanjani tuu. Mascout wanaangalia maisha ya nje ya uwanja ya mchezaji, ni nini anapenda, ni nini hapendi, Namna anavyoishi na wenzake na hata maisha yake ya Ndani kabisa.

Halafu kisha ndo wanaangalia Kiufundi anaifaa timu? je timu inaweza kukidhi gharama zake? kama haiwezi, basi wanatafuta mchezaji mwingine mwenye sifa hizo alafu klabu inaweza kumpata. Tatizo linaanzia hapa, je timu zetu zinamascout? jibu ni hapana.

Yanga

Kwa namna Ambavyo Carlinhos anacheza kiwanjani, naamini haikuwa sahihi kuja kucheza Tanzania. Ligi yetu ina migongano mingi sana viwanjani, viwanja vyenyewe vibovu, hivyo inahitaji Mchezaji mwenye Fitness ya hali ya juu.

Kama Vilabu vyetu vingekuwa na Uwezo wa kufanya Scouting, basi kuna sajili zisingekuwa zinafanyika. Scouting inaishia kwenye Video za Youtube tu.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa