Yanga Vs Simba Yamebaki Masaa Machache

Mashabiki wa soka nchini wapo kwenye hekaheka za kusubiri pambano kubwa zaidi la mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu, Dabi ya Kariakoo, ambapo vigogo wa Tanzania Bara, Yanga SC na Simba SC, watakutana Septemba 16, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Huu ni mchezo wa kugombea Ngao ya Jamii, taji linaloashiria ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26. Kwa mujibu wa ratiba, imebaki siku moja tu kabla ya wapinzani hawa wa jadi kupanda dimbani kuonyesha ubabe.

Yanga Vs Simba Yamebaki Masaa Machache

Msimu wa 2024/25, Ngao ya Jamii ilichukuliwa na Yanga SC, baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Azam FC katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Mkapa. Simba SC wao hawakufika fainali, baada ya kung’olewa na Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na Maxi Nzengeli.

Safari ya kuelekea dabi hii imepambwa na ushindi wa michezo ya kirafiki ya kimataifa. Simba SC walionyesha ubabe wao Septemba 10, 2025 kwenye kilele cha Simba Day, baada ya kuichapa Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0. Siku mbili baadaye, Septemba 12, 2025, Yanga SC nao hawakubaki nyuma, wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari FC ya Kenya, katika kilele cha Yanga Day.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yanga Vs Simba Yamebaki Masaa Machache

Mashabiki wanatarajia pambano lenye hadhi kubwa, likibeba hisia za ushindani wa jadi wa zaidi ya miongo saba. Kwa Simba, ni fursa ya kulipiza kisasi cha msimu uliopita na kufungua ukurasa mpya kwa kishindo. Kwa Yanga, ni nafasi ya kuthibitisha uimara wao na kuendeleza rekodi nzuri ya karibuni dhidi ya watani wao.

Kwa kila upande, ushindi katika mchezo huu ni zaidi ya taji kwani kila mmoja anataka kumuonyesha mwenzake kwamba yeye ni bora zaidi kuelekea msimu mpya huku bingwa akitegemewa kuanza ligi vizuri akiwa na morali ya juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.