Alisema Nicolas Pepe wa Arsenal “kama hauchezi, hauwezi kuwa na furaha”. Olivier Giroud anapitia hayo ndani ya Chelsea, Frank Lampard anasisitiza kumuhitaji mshambuliaji huyo licha ya kusugua benchi kwa muda mrefu.

Giroud anatazamia kufanya maamuzi mapema mwezi Januari endapo hali yake haitobadilika ndani ya kikosi cha Chelsea kwa siku zilizobaki kabla ya dirisha jipya kufunguliwa rasmi.

Hii ni baada ya Kocha wa Chelsea – Frank Lampard kutompa nafasi Giroud kuonesha uwezo wake na zaidi sana anamtumia kama ‘super sub’ kitu ambacho mshambuliaji huyo akubaliani nacho.

Giroud alifanya vizuri sana mwishoni mwa msimu uliomalizika na kuisaidia Chelsea kumaliza kwenye nafasi ya 4 kwenye msimamo wa EPL. Akiwa na timu ya Taifa ya Ufaransa katika Mashindano ya UEFA Nations League, alianza katika mechi 2 kati ya 3 na kupachika magoli 2 katika mchezo dhidi ya Sweden.

Frank Lampard, Frank Lampard Anamuhitaji Giroud, Meridianbet
Olivier Giroud Akiwa na Timu ya Taifa ya Ufaransa.

Hali ni tofauti msimu huu ndani ya kikosi cha Frank Lampard ambapo Timo Werner na Tammy Abraham wanapewa nafasi zaidi ya kuongoza safu ya mashambulizi ya Chelsea na Giroud akitumika kama mbadala wa wachezaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lampard amesema “Nina mipango na Oli. Ni mchezaji wa muhimu kwenye kikosi chetu.

Frank Lampard, Frank Lampard Anamuhitaji Giroud, Meridianbet
Olivier Giroud akipachika goli kwenye mchezo dhidi ya Norwich City msimu wa 2019/20. Ushindi uliowapa Chelsea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa 2020/21.

“Alikuwa wa muhimu sana mwaka jana. Alicheza michezo mingi na alianza kwenye michezo hiyo. Kila siku atahitaji kucheza zaidi na ni mchezaji wa muhimu sana kwenye timu.

“Ninajua ataendelea kuwa mchezaji wa muhimu kwetu kwahiyo ninataka Oli abaki hapa. Ninamahusiano mazuri na Oli na kama alijisikia kwa namna yeyote kwamba hili litabadilika basi nitafurahi kama nitafanya haya mazungumzo na yeye.

“Lakini ninamtaka abaki hapa. Nipo tayari kwa lolote litakalotokea kama kutakuwa na mabadiliko yeyote lakini kwa sasa ni mchezaji wa muhimu kwetu.”


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

24 MAONI

  1. Inavyoonekana kocha Frank Lampard anamuhitaji sana mchezaji Giroud labda anaumuhimu nae badae sema tu mchezaji hajamuelewa kutokana na kuwekwa benchi kwa muda ampe tu nafasi nafikiri kocha anaumuhimu mkubwa kwake

  2. Giroud inabid ajaribu kuangaliah utaratibu wa kuhama chelsea na kutafuta timu yakucheza mara kwa mara ilihawez kukuza kiwango chake na kurudi kwny ubora wake Kama giroud tuliyomzoeha wa kipind hcho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa