Licha ya kutawala mchezo kwa kipindi kirefu, Frank Lampard alishuhudia vijana wake wakiambulia pointi 1 dhidi ya Tottenham Hotspurs wikiendi hii.

Juhudi za kutafuta magoli ziligonga mwamba kwa timu zote mbili huku makipa wa timu hizi wakionesha uwezo mkubwa wa kulinda magoli yao. Baada ya mchezo huo, makocha walikuwa na yao ya kusema.

Jose Mourinho alinukuliwa akisema “hata hatupo kwenye mbio kwa hiyo sisi sio farasi. Sisi ni wadogo, farasi wadogo na mnaona utofauti.”

Frank Lampard alienda mbali zaidi na kusema ” hayo ni maneno ya Jose kama anavyoona yeye lakini kwa nje tunaona, wao ndio wanaongoza ligi, ni mpishano mdogo sana kwenye nafasi za juu.

“Kama sisi tunawania ubingwa basi na wao wanawania ubingwa. Ukiwa na Harry Kane pamoja na Son kwenye timu – Son anamagoli 9 na Kane 7, wanaweza kulinda goli lao kutokana na namna wanavyojipanga, lazima wanatarajia kuwa miongoni mwa wanaowania ubingwa.

“Wamewekeza sana,wana wachezaji kama Gareth Bale kwenye benchi, Dele Alli hakuwepo kabisa hapa. Wanakikosi kizuri. Ninadhani wote tunawania ubingwa, Jose atasema kwa namna anavyoona yeye.”

Tottenham wamerejea kileleni wakiwa na pointi 21 sawa na Liverpool ila wanaongoza kwa tofauti ya magoli 7. Vijana wa Frank Lampard – Chelsea wanashika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 19.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Frank Lampard, Frank Lampard: Spurs Wanawania Ubingwa., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa