Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amepigwa faini ya £30,000 kwa kumkosoa mwamuzi aliyechezesha mchezo wa Everton dhidi Liverpool  mwezi uliopita kwa kumshtumu mwamuzi huyo kuwa pendelea majogoo kwenye mchezo huo ambao walipoteza.

Mapema mwezi huu, chama cha soka nchini uingereza FA, walimfungulia mashitaka kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard kwa tabia mbovu aliyoionyesha ya kumshambulia mwamuzi na kutokua na imani na maamuzi aliyoyafanya kwenye wa derby ya Merseyside.

Frank Lampard

Frank Lampard alipinga mashataka na sasa amepigwa faini ya “kuvunja kanuni ya FA E3, alipokuwa akifanya mahojiano na vyombo vya habari, imethibitishwa katika kikao chao pamoja nae kwenye usikilizwaji wa kesi yake.” Waraka wa FA ulisema.

“Kocha wa Everton Frank Lampard, amepinga kwamba hakuvunja kanuni ambayo inahusika na kumtenga au kutokuwa na imani na mwamuzi wa mchezo au waamuzi kwa ujumla au kuleta sintofahamu kwenye mchezo au kuingili mchezo, kulingana na sheria ya FA E3.1.” FA waliongozea

Frank Lampard akichukua hatamu ya kuinoa klabu ya Everton mwezi January ambapo klabu hiyo ilikuwa kwenye nafasi za kushukua daraja, lakini Lampard amefanikiwa kuingoza mpaka nafasi ya 16 na kuhakikisha wanabaki ligi kuu ya Uingereza kwa msimu ujao.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa