Fred Aaga Manchester United

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Brazil Fred Rodrigues ameaga rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano.

Kiungo Fred ambaye alijiunga na Man United mwaka 2018 akitokea Shakhtar Donetsk amefanikiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.fredKiungo huyo wakati anaandika waraka wake wa kuaga klabuni Man United ameeleza anajivunia miaka mitano ndani ya Man United kwani klabu hiyo ni moja klabu kubwa kabisa ulimwenguni na kwake ilikua ni ndoto iliyotimia kuitumikia timu hiyo.

Katika lile fagio ambalo Manchester United walipanga kulifanya katika majira haya ya kiangazi limempitia na kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil, Lakini hatakua wa mwisho kwani kuna wachezaji wengine kadhaa watamfata.fredKiungo Fred Rodrigues anaondoka Manchester United akiwa amefanikiwa kubeba taji moja ambalo ni kombe la Carabao, Lakini zaidi atakumbukwa zaidi kwa kujitoa kwake asilimia 100 pale ambapo anakua anahitajika na timu yake.

Acha ujumbe