Rafael Nadal amefika fainali yake ya 14 ya French Open baada ya Alex Zverev kutolewa nje ya uwanja kwenye Wheelchair katika nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo.
Mchezaji bora namba 3 wa dunia, Zverev alipata majeraha ya kifundo cha mguu katika kona ya uwanja ambapo alikuwa akitaka kuucheza mpira katika uwanja wa Philippe Chatrier.
Katika nusu Fainali ya pili ya French Open, Casper Ruud alipata ushindi dhidi ya Marin Cilic kwa seti 3-6, 6-4, 6-2 na 6-2 na kuwa Mnorway wa kwanza kutinga fainali ya Grand Slam.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!