Klabu ya Manchester United Imekubaliana na Barcelona kuhusu uhamisho wa kiungo wake Frenkie de Jong baada ya mazungumzo ya muda mrefu, huku ikatarajiwa United kulipa kiasi cha €85milioni lakini mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Uholanzi amegoma.

Frenkie de Jong hana nia ya kuondoka kwenye klabu ya Barcelona kwa sasa, licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji ambao mishahara yao itapunguzwa ili kuweza kuisaidia klabu hiyo kujikwamua na mzigo mkubwa wa bill za mishahara.

Frenkie de Jong, Frenkie de Jong Ndio Kikwazo kwa Manchester United, Meridianbet

Makubalino binafsi bado tatizo ambalo klabu zote mbili zinahitaji kulitua kwa sasa, ili kuweza kumshawishi De Jong kumwaga wino na kumfuata kocha wake wa zamani ambaye alifanya nae kazi katika klabu ya Ajax.

Frenkie de Jong alisajiriwa na klabu ya Barcelona 2019 kwa uhamisho uliogharimu €75million, ambapo awali kulikuwa na tetesi kuwa angejiunga na klabu kati  Manchester United Manchester City na Paris Saint-Germain

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa