Klabu ya Fulham FC imefanikiwa kurejea katika Ligi kuu ya Uingereza EPL baada ya hapo jana kupata ushindi wa magoli 3-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Preston katika mchezo wa Championship.
Ushindi huo unamfanya Fulham FC iliyoshuka kutoka Ligi Kuu ya England mwaka 2021 kufikia alama 86 ambazo haziweza kufikiwa na wapinzani wake wakiwa wamebakia na michezo 3.
Magoli ya mawili ya Aleksandar Mitrovic dakika ya 9′ na 41′ na lile la Fabio Carvalho dakika ya 34′ yaliwahakikishia ushindi katika kipindi cha kwanza katika dimba la Craven Cottage.
Tangu msimu wa mwaka 2018/19 ilipopanda daraja hadi msimu ujao wa 2022/23 inapopanda tena, Fulham imepanda EPL mara 3 na kushuka mara 2.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.