Fulham Mbioni Kumpoteza Harvey Elliott

Fulham wapo mbioni kumpoteza kinda ambaye alikuwa kwenye rekodi kama kijana mdogo zaidi kucheza ligi Ligi Kuu ya Uingereza Harvey Elliott baada ya kinda huyu kukataa kusainisha mkataba mpya.

Fulham ambao wameshuka kushiriki Championship watapata hasara ikiwa staa huyu hatasaini dili jipya. Klabu hii walikuwa na mpango wa kukinoa kikosi chao na kubaki na vijana wao bora tayari kupambana msimu ujao.

Sakata la Harvey Elliott kukataa mkataba mpya limewapa upenyo klabu za Real Madrid na Barcelona, zinadaiwa kumtupia macho kinda huyu tayari kwa kumkwapua ikitokea tu Fulham wakishindwa kumshawishi kusaini.

Kinda huyu alicheza gemu yake ya kwanza ya EPL dhidi ya Wolves, thamani yake ingefikia paundi milioni kadhaa kama Fulham wakifanikiwa kuinasa saini yake na kutaka kumuuza baadaye. Lakini mpaka sasa vilabu vinavyomfukuzia vinaweza kumnasa kwa paundi laki 2 tu.

Acha ujumbe