Muendelezo wa ngekewa kwa klabu ya Fulham kwa misimu minne mfululizo umeendelea tena msimu huu. Walipanda, wakashuka, wakapanda tena, wameshuka tena daraja.

Vijana wa Scott Parker wameshuhudia safari yao ya kuendelea kusalia EPL msimu ujao ikihitimishwa wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Craven Cottage.

Ushindi wa magoli 2-0 kwa Burnley, umewafungasha virago Fulham zikiwa imesalia michezo 3 msimu huu kumalizika. Hii ni historia kwenye EPL kwa timu 3 zinazoshuka daraja, kujulikana kabla ya msimu haujaisha na zikiwa zimesalia mechi 3.

Kabla ya Fulham, West Brom Albion na Sheffield United zilishathibitika kushuka daraja na sasa ni rasmi, timu hizi hazitokuwepo kwenye EPL msimu ujao. Ukisikia mgeni njoo, mwenyeji apone ndio kinachotokea kwenye EPL na Championship.

Fulham, Fulham Rasmi Kushuka Daraja Msimu Ujao., Meridianbet
Magoli kutoka kwa Ashley Westwood na Cris Wood yalitosha kuwashusha daraja Fulham na kuwanusu Burnley msimu huu.

Wakati watatu wakishuka, watatu wanapanda EPL msimu ujao. Norwich City na Watford walishuka daraja msimu uliopita na wameenda kufanya makubwa kwenye Championship mpaka kupata nafasi ya kurejea kwenye EPL msimu ujao, sambamba na vilabu hivi, Bournemouth wanaweza kuungana nao endapo watafanya vizuri kwenye michezo ya mtoano.

Baada ya mchezo dhidi ya Burnley, kocha wa Fulham (Scot Parker) amenukuliwa akisema “tunahitaji kujaribu na kujinasua kwenye huu muenendo tulionao. Lakini sasa hivi sio muda sahihi wa kusema tunafanyaje kwenye hilo. Ninadhani ninafahamu hilo linawezekanaje, lakini huu sio muda wa kulisema kwa upana zaidi.”

Swali ni Je, Scot Parker ataendelea kukinoa kikosi hicho ambacho alikipandisha daraja msimu uliopita na anashuka nacho daraja msimu huu au ndio anawaacha vijana wake?


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Fulham, Fulham Rasmi Kushuka Daraja Msimu Ujao., Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa