Klabu ya Manchester City inaangalia uwezekano wa kufanya usajili katika safu yao ya ulinzi ili kuwa na wachezaji ambao watakuwa na msaada katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na changamoto ya wachezaji wa nafasi hiyo kwa kuwa na majeruhi wengi. Kwa sasa jicho lao ni kwa nyota wa Benfica ambaye pia anawindwa na klabu ya Manchester United, Ruben Dias.
Kwa sasa United inataka kufanya usajili mzito wa nyota nane ndani ya misimu miwili ijayo ndani ya kikosi hicho na tayari wameweza kuwaweka mezani wale wanaotazamia kuweza kuwasajili klabuni hapo. inasemekana wametenga kitita kinono ili kuweza kuwashawishi Leicester City juu ya kuwasajili nyota wake wawili ambao ni Maddison na Chilwell. Watakutana na upinzani kutoka kwa Chelsea ambayo inaonekana kumhitaji Chilwell wakipata idhini ya kusajili.
Klabu ya Tottenham inafikiria kufikia maamuzi ya mapema ili kumuuza nyota wake na kiungo raia wa Denmark, Eriksen ambaye amekuwa akitupiwa jicho na klabu ya Real Madrid kwa kipindi kirefu. Raia huyo wa Denmark anaelekea katika kipindi cha mwisho cha mkataba wake na kikosi hicho lakini haoneshi dalili ya kuendelea kusalia klabuni hapo hivyo ili yasitokee mapungufu ya kumruhusu kuondoka bure wanaona ni bora wampeleke sokoni. Mbali na kuhusishwa kwake na Madrid ambako Rais wa klabu hiyo hatamani kabisa kumpoteza kwa namna yoyote anafikiria kumpeleka nyota huyo. Nyuma ya pazia, kocha wa klabu hiyo bado mapendeleo yake yapo kwa kiungo wa United, Paul Pogba ambaye anahisi ni mtu muafaka kuwa naye klabuni hapo. Mbali na hilo anafaa kabisa kuwa katika klabu kubwa kama hiyo na kufanya naye kazi.
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ametupilia mbali taarifa zilizomhusisha yeye kujiunga na klabu ya Lyon ili kuifundisha na kusema kwamba hana mpango wa kutua klabuni hapo kwa sababu ana klabu ambayo anategemea kuifundisha. Mbali na hilo hajaweka wazi juu ya klabu ipi sasa anatazamia kuifundisha mara baada ya kuwa nje ya ukufunzi kwa kipindi kirefu hadi sasa.
Klabu ya Arsenal ipo mbioni kufukuzia usajili wa nyota wa Feyernoord ya Uholanzi, Orkun Kokcu ili kuona kama wanaweza kuwa naye ndani ya klabu yao. Pia, wapo katika harakati za kuangalia kama wangeweza kumtoa kwa mkopo kiungo wao, Mesuit Ozil akaweza kujiunga na klabu ya Fernabhce.
Povel tz
Gud news