Fununu za Soka Barani Ulaya

Klabu ya Liverpool ipo katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba nyota wa klabu hiyo, Sadio Mane ambao kwa sasa utakuwa mnono zaidi na wanatazamia kuanza kumlipa nyota huyo kiasi cha £220,000 kwa wiki ambayo ni ongezeko kubwa kutoka kwenye kiwango ambacho alikuwa anakipokea hapo awali ndani ya klabu hiyo ya Majogoo hao wa Uingereza.

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania, David Silva [33] anatazamiwa kujiunga na klabu inayomilikiwa na mchezaji wa zamani, David Beckham inayojulikana kama Inter Miami pindi tu mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Manchester City utakapofikia ukingoni. Nyota huyo atakuwa huru kufanya kazi na nyota huyo wa zamani wa soka aliyehudumu klabu mbalimbali.

Mchezaji wa Inter Milan aliyejiunga kutoka Manchester United, Romelu Lukaku na mchezaji ambaye alikuwa kikosini hapo, Brozovic inasemekana waligombana katika vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mechi yao kuisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Slavia Prague siku ya Jumanne na baadaye ugomvi huo kuamuliwa na nyota mwezao, Alexis Sanchez aliyeona hakuna haja ya wawili hao kugombezana.

Baada ya kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Valencia nyota wa klabu ya Chelsea, Mount kutokana na ripoti ya madaktari inaonekana kwamba hakupata majeraha makubwa sana ambayo yanatisha kwake kwamba angekaa nje kwa kipindi kirefu. Hiyo ni ahueni kwa Lampard kwa sasa kwa sababu atampata nyota huyo kikosini kwake mapema sana.

Leicester City wapo sokoni kufukuzia wachezaji ambao wanaona kwamba wataweza kuwa na msaada mkubwa sana kikosini kwao kwa siku za mbeleni. Hadi sasa taarifa za awali zinasema kwamba wameanza kumchunguza mchezaji wa Benfica, Almeida ambaye wanaamini kabisa kwamba anafaa kuwa ndani ya kikosi chao.

Wanasema furaha ya kuwa sehemu fulani hupelekea kufanya makubwa sehemu husika, nyota wa klabu ya Liverpool ambaye alisikika siku za karibuni akisema kwamba anafikiri kuondoka kikosini hapo kutokana na kukosa muda wa kucheza uwanjani jambo ambalo hakubaliani nalo, anasema kwamba pamoja na hilo anafurahia sana maisha ya kuwa kikosini hapo.

Kumekuwa na vurugu za mashabiki wa klabu ya Real Madrid kumtaka kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane aweze kuondoshwa kikosini hapo, basi maamuzi hayo yakifikiwa klabu hiyo itatakiwa kumlipa kocha huyo fidia ya kiasi cha £80m ili aweze kuachia wadhifa huo.

Acha ujumbe