Huenda klabu ya Bayern Munich ikaingilia biashara ya klabu ya Real Madrid juu ya usajili wa nyota wa klabu ya Tottenham ili kujenga kikosi chao. Kikosi hicho cha Bayern kinaangazia kama kuna kila linalowezekana ili kuweza kuingilia biashara hiyo ya usajili kikosini hapo kwa siku za mbeleni. Eriksen anaonesha nia ya kuihama klabu yake hiyo na kujiunga na klabu nyingine siku za mbeleni.
Wolves wana nia kubwa ya kupata usajili mwingine ndani ya kikosi chao na kuna kila dalili kwamba wakaweza kumsajili raia wa Congo, Luyindama anayesakata soka lake kunako klabu ya Galatasaray. Klabu hiyo inahusishwa na nyota huyo ikiwa ni malengo yao ya kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo ili kujiweka pazuri ndani ya ligi yao.
Manchester United wanaonekana wanamaanisha kweli juu ya usajili wa nyota wa klabu ya West Ham, Rice ambaye wamekuwa wakimzungumzia kwa kipindi kirefu sana. Nyota huyo amekuwa na kiwango cha aina yake ndani ya taifa hilo na ndani ya klabu hiyo, kutokana na kiwango chake anawashawishi United kufungua kitita kikubwa kutokana na uhitaji wao wa wachezaji. Mbali na hayo kocha wa klabu hiyo ameushauri uongozi wa klabu hiyo kuhusiana na masuala ya kiusajili ya kwamba ni vyema wakawa na mfumo wa kutumia taifa la Hispania kama washauri wao wa masuala ya usajili na katika jukumu zima la kuajiri kutokana na uzoefu wa taifa hilo. Anaamini kupitia hilo watafanya mambo sahihi.
Marcus Rashford na Harry Kane ni kati ya Waingereza wawili wanaowindwa na klabu ya Barcelona. Miamba hao wa soka kwa hakika wamekuwa sehemu ya mategemeo ya kikosi hicho ambacho kinafikiria kuwapa namba wachezaji hao kama wakikubali kujiunga na klabu yao. Barcelona kwa sasa wapo mbioni kuangalia juu ya nani anayeweza kukaa katika nafasi hiyo jambo ambalo linawapa kasi ya kutafuta wengine kutokana na umri wa Suarez kusogea sana.
Manchester City wanategemewa kukaa mezani na kiungo wa muda mrefu wa kikosi hicho, Fernandinho kukubaliana naye kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia kikosini hapo kwa miezi 12 mingine. Matajiri hao wa jiji la Uingereza hawaoni ugumu kuendelea kuwa na nyota huyo kutokana na uwezo wake na kiwango chake cha pekee, pia, mchango wake mkubwa ambao ameuonesha ndani ya klabu hiyo.
Furahav
Nenda tu.