Wakati mapazia ya ligi nyingi yakielekea kufunikwa tayari klabu nyingi zimeanza kujiandaa kufanya usajili ndani ya vikosi vyao jambo ambalo huwa na umakini wa aina yake na lazima klabu zenye vigezo vya kufanya hivyo zijiimarishe zaidi kwa msimu wa ushindani ujao pale walipokosea msimu uliopita.
Sakata linaloendelea ndani ya klabu ya Barcelona ni kuhusiana na Coutinho ambaye wengi wanaamini sio mchezaji mwenye damu ya Kikatalunya na haendani na falsafa ya kuendelea kuwa na miamba hao. Na baada ya matajiri hao kutolewa katika michuano ya klabu bingwa tatizo limezidi kuwa kubwa zaidi kwa nyota huyo kuonekana haendani kabisa na falsafa zao.
Kinachoendelea ni kama nyota huyo atauzwa huku wakitenga dau la hasara kabisa tofauti na ile waliyotumia wao kumnunua nyota huyo. Kuna uwezekano akatua katika klabu zilizokuwa zinamfukuzia kwa kipindi kirefu kama United. Mbali na nyota huyo ndani ya klabu hiyo, bodi ya wamiliki wa klabu kwa sasa wanafikiria pia suala la kocha wa klabu hiyo kama anastahili kuendelea kusalia hapo au kuachia nafasi kwa wengine.
Valverde alitupwa nje na kikosi chake ikiwa ni mara ya pili kwake kukutana na tatizo hilo. Na taarifa za chini ni kuwa kocha wa Ajax ameanza kuhusishwa kutua klabuni hapo tayari. Nyota wengine waliopo mbioni ni Rakitic na Umititi.
Nyota wa michuano ya klabu bingwa, Origi amezawadiwa kandarasi ya miaka miwili ndani ya klabu hiyo kutokana na uwezo wake aliouonesha na klabu hiyo imeridhika kabisa na uwezo wake hadi kuamua kumzawadia mkataba huo mnono wa kuendelea kusalia klabuni hapo. Wameamua kufanya hivyo ili kuziba mianya ya tamaa iliyokuwa imeanza kuonekana ya klabu nyingine kumhitaji.
Safari ya Eden Hazard kuelekea Real Madrid ilionekana kuingiwa na mdudu kutokana na klabu ya Chelsea kupigwa kufuli la kusajili ambapo kwa sasa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili msimu huu na hata ujao jambo ambalo lilionekana litakuwa gumu klabu hiyo kumruhusu mchezaji huyo aondoke sasa. Hilo linaweza kuwa kikwazo sana kwa Real Madrid ambao wamemfukuzia kwa kipindi kirefu sana nyota huyo.
Nyota wa Madrid, Bale anatamani kuendelea kusalia kikosini hapo pamoja na kwamba sio mapendeleo makubwa ya kocha wa klabu hiyo kwa sasa kutokana na uwezo wake kushuka kabisa. Wakala wa mchezaji huyo, Jonathan Barnett anaonelea kwamba mchezaji wake anatamani kuendelea kusalia hapo lakini anapata walakini kutokana na mapendeleo ya Zidane kama atahitaji kusalia na nyota huyo. Staa huyo bado ana mkataba unaompa nguvu ya kuwa hapo hadi 2022.


Furahav
Hongereni kwa usajir
Janeflora malisa
Good
Povel
Habar njema
Lydia Emmanuel Magoti
Habari njema
Furahav
Habari safi