Willian sokoni tena, klabu za Hispania ambazo ni Barcelona na Atletico ziko mbioni kujaribu kuwashawishi Chelsea kama wanaweza kumuachia nyota wa kikosi hicho baada ya kuridhishwa na kiwango chake cha kipekee. Raia huyo wa Brazil, kwa nafasi kubwa, amekuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho wakati wote anapopata nafasi ya kuingia uwanjani. Kwa sasa Barcelona wanaonekana kuanza kuonesha mapendeleo yao juu ya nyota huyo kwa kuangalia kama wanaweza kumnasa. Wote wameweka mezani kitita cha Β£35m kama ada ya awali kumfukuzia lakini kwa hali halisi ni vigumu biashara hiyo kufanyika.
Matthijs de Ligt kutua United? Taarifa zinazoendelea ni juu ya nani atafanikiwa kunasa saini ya mlinzi huyo mwenye umri mdogo sana ambaye amekuwa na makali ya pekee sana ndani ya ligi. Mchezaji huyo amekuwa akifukuziwa na Barcelona vilevile United ambao wana nia dhahiri ya kuimarisha kikosi chao kwa sasa. Pamoja na mapendeleo ambayo Barcelona wanayaonesha juu ya nyota huyo lakini kwa nafasi yao lakini kwa mchezaji ambaye anahitaji nafasi kubwa ya kucheza kama huyu wana nafasi ndogo sana ya kumnasa kutokana na kikosi chake na aina ya wachezaji alionao hivyo United wana nafasi zaidi.
Eljif Elmas kutua Spurs, Pochettino mara nyingi hana kawaida ya kuwa na kelele sana wakati anafanya usajili wake na mara nyingi husajili wachezaji ambao sio rahisi kuamini kama wataweza kuwa na hatari kwa baadaye. Kwa sasa amemuweka kwenye rada zake mchezaji huyo wa Fenerbahce ili aweze kumnasa ndani ya kikosi chake. Mchezaji huyo, kwa takwimu, amekuwa na nafasi ya pekee ndani ya klabu yake na kama atanaswa na Spurs utakuwa ni wakati wake wa kuuza zaidi.
West Ham watafutwa na United, ni katika biashara ya kutaka kumnasa nyota wao anayekipiga ndani ya kikosi hicho kwa mafanikio makubwa sana. Kwa sasa wamejaribu kuwashawishi Wagonga Nyundo hao kama wanaweza kufanya biashara ya kumnasa Issa Diop ambaye amekuwa na msimu wa pekee sana ndani ya kikosi hicho. Japo West Ham wanaonekana hawapo tayari kumuachia nyota huyo kwa sasa. Ila lolote hutokea endapo mchezaji mwenyewe ataamua kuwa na maamuzi binafsi akashinikiza klabu yake.
Maurizio Sarri asuka mipango, baada ya kusaini miaka mitatu ya kuifundisha Juventus kwa sasa kocha huyo ameweka mezani wachezaji wawili anaotamani kufanya nao kazi kwa wakati uliopo. Wachezaji hao ni Jorginho na Emerson ambao ameona uwezo wawe ndani ya kikosi cha Chelsea, hivyo anatamani sana kama angewaondoa kikosini hapo.
Povel
Habar njema