Kuna kila dalili kwamba United walitumia mbinu kubwa sana kumpeleka mlinzi wao ambaye kwa msimu uliopita alikuwa ni tegemeo sana ndani ya kikosi chao hicho. Kwa taarifa zaidi juu ya nyota huyo ni kwamba huenda akaendelea kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa kipindi kirefu sana zaidi ya vile ilivyokuwa awali kwamba angesalia kwa msimu mmoja pekee. Lakini kuna kila dalili kwamba akapewa muda zaidi kwa misimu miwili ya kuwa na kikosi hicho cha Roma kwa mkopo.
Msimu wa Januari utarudi kwa kasi ile ile ya klabu kuingia sokoni kupigania majina ambayo watataka kusajili uwanjani ili kuvipa nguvu vikosi vyao. Hadi sasa Inter Milan na Manchester United wanaonesha nia yao kutaka kupigania nafasi ya kumsajili nyota wa Tottenham, Eriksen ambaye mipango yake ya msimu huu imefukiwa na kushindikana kuhama klabuni hapo kuelekea Hispania.
Wachezaji Emre Can, Mario Mandzukic na Chiellini wamewekwa nje ya kikosi cha Juventus kitakachoshiriki katika kampeni za awali katika kutafuta nafasi ya kushiriki klabu bingwa Ulaya. Ndani ya majina ambayo yanetolewa na klabu hiyo kwa ajili ya hatua za mwanzo za kusaka tiketi ya mashindano hayo watatu hao waneweza kuachwa kushiriki kwenye kampeni hiyo, hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho.
Maurizio Sarri, ambaye kwa sasa anainoa Juventus, ameweka bayana malengo yake ya kutaka kumnasa mchezaji wake wa zamani ambaye amefanya naye kazi ndani ya kikosi cha Chelsea, Willian. Kocha huyo anatamani sana kufanya kazi na nyota huyo kwa mara nyingine baada ya kuweza kumtumia sana kwenye mechi nyingi alipokuwa kocha ndani ya Chelsea. Japo kimfumo nyota huyo hana utofauti kiuchezaji na Costa huenda ni mapendeleo tu ya kocha.
Tutegemee kumuona Wenger akirejea kwenye benchi lake kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita ambapo alikuwa akifundisha ndani ya klabu ya Arsenal. Kocha huyo anayetazamia kutimiza miaka 70 hivi karibuni ametangaza nia yake ya kutaka kurejea uwanjani siku za hivi usoni ikiwa ni sehemu ya yeye kuendeleza historia yake uwanjani japo bado hajasema kwamba safari yake hiyo itakuwa ndani ya klabu gani kwa sasa.
Imebainika kwamba nia ya Bayern Munich kumsaini mchezaji wa Manchester City iliweza kupotea ghafla mara baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano sahihi ya mshahara ambao wangeweza kumlipa nyota huyo kama sehemu ya makubaliano yao. Jambo hilo ndilo lililokwamisha usajili wa nyota huyo kutua kwao Ujerumani ndani ya Bayern.
Povel
Habar njema