Tazama wasifu wa Gael Bigirimana, alikuwa na nafasi kubwa ya kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Nasradine Nabi, kwa sababu miaka ya nyuma Soka la Tanzania lilikuwa sehemu ya wachezaji wa kigeni kucheza kwa urahisi sana ukilinganisha na uwezo wao, yaani kwa mchezaji mwenye CV na sifa kubwa alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuingia kikosini moja kwa moja bila hata kuzingatia ubora wake.

Uwezo wa Bigirimana Bado Haujamridhisha Nabi.

Mechi dhidi ya Vipers SC alitokea benchi, game dhidi ya Simba SC Fainali ya Ngao ya Jamii hakucheza kabisa, alianza dhidi ya Polisi TZ na hakumaliza mechi. Alitolewa.

gael, Gael Bigrimana Mambo Magumu Yanga Sc., Meridianbet

Game dhidi ya Coastal Union aliingia dakika za 80 hivi. Sio kama sio bora hapana, kuna utajiri wa viungo wenye uwezo mkubwa pia pale Yanga ndiyo maana inakuwa ngumu sana kwake kupata nafasi ya moja kwa moja, na huenda ikamchukua muda sana hadi kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza.

ukiitzama safu ya viungo ya Yanga unaona namna ambavyo imetawaliwa na viungo wenye uwezo mkubwa mno, kama Khalid Aucho, Salum Aboubakar, Yannick Bangala na Feisal Salum. Kwa upande mwingine nafikiri bado anaendelea kutafuta utimamu wa mwili (fitness) zaidi kwa sasa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa