Cody Gakpo ametoa kidokezo chake kikubwa zaidi cha uhamisho kwa kukiri kuwa anafikiria kuhamia Manchester United msimu huu wa dirisha dogo la usajili la Januari.
Gakpo mwenye umri wa miaka 23, na mchezaji wa timu ya Taifa ya Uholanzi sasa ana thamani ya zaidi ya pauni milioni 50 baada ya kung’ara kwenye Kombe la Dunia kwa kufunga mabao matatu katika mechi za hatua ya makundi.
Yeye na wachezaji wenzake wa Uholanzi wanakabiliwa na mechi ngumu ya hatua ya robo fainali na Argentina kesho jioni lakini mjadala kuhusu mustakabali wa klabu hiyo tayari umeanza.
Katika mahojiano ya wazi na chombo cha habari cha Uholanzi NRC, Gakpo amezungumzia kusikitishwa kwake kwa kutopata uhamisho wa Ligi Kuu msimu uliopita, pamoja na kutoa mawazo yake kuhusu uwezekano wa kuhamia Old Trafford alisema kuwa alifungua uamuzi wa dakika za mwisho wa kukataa kwenda Leeds mwezi Agosti.
Gakpo alisema: “Hicho kilikuwa kipindi kikali. Nilijifunza kutokana na hilo. Nitafanya mambo kwa njia tofauti sasa, nilifikiria kuhusu Manchester United lakini hilo halikufanyika, sikujua zaidi na niliaznza kuwa na mashaka.”
Leeds walikuja lakini alijiuliza aende huko? lakini akaona hapana na anasubiri kuona kila kitu, kwani bado hajasikia kutoka kwa United na wakija nitafikiria juu yao. Katika maamuzi hayo pia anasema kuwa atatafuta msaada wa Mungu amuulize kile anachoweza kufanya vizuri zaidi.
Inafikiriwa kuwa Jesse Marsch wa Leeds walikuwa na ofa iliyokubaliwa kwa ajili ya Gakpo lakini hawakuweza kumfanya mchezaji huyo kukubaliana na masharti ya kibinafsi, huku kocha huyo akisema kuwa mwezi uliopita dili limekamilika 99.9%, lakini anaamini uchezaji wa mchezaji huyo katika Kombe la Dunia sasa umemtoa kwenye bei ya klabu hiyo ya West Yorkshire.
Wakati huohuo, Mashetani Wekundu wamekuwa wakihusishwa na kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa miezi kadhaa, huku Erik ten Hag akitambulika kama kumkubali nyota huyo wa PSV Eindhoven.
Akiwa tayari amewaleta Tyrell Malacia na Antony Old Trafford kutoka Eredivisie, kocha huyo amejidhihirisha kuwa mwamuzi mwerevu wa talanta hadi sasa na mpango unaonekana kutozuilika.