Gallagher Kutimkia Atletico Madrid

Kiungo wa klabu ya Chelsea Conor Gallager anaelezwa kuwindwa kwa karibu na klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Atletico Madrid wanaelezwa kumfatilia kwa karibu sana Gallagher na yupo kwenye orodha yao juu kabisa kwenye wachezaji ambao wanawataka kwenye dirisha hili, Hivo mabingwa hao wa zamani wa Hispania watahakikisha wanaipata saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza.gallagherKlabu ya Chelsea wanaelezwa kuhitaji kiasi cha €milioni 35/40 kutoka kwa klabu ya Atletico Madrid ili waweze kumuachia kiungo Conar Gallagher, Hivo miamba hiyo ya soka nchini Hispania ndio wapo kwenye mazungumzo kwasasa na Chelsea kwajili ya kuhakikisha wanafikia makubaliano ya kupata saini ya kiungo huyo.

Klabu ya Atletico Madrid wanaelezwa wako kwenye mkakati wa kuhakikisha ndani ya wiki hii wanakamilisha saini ya kiungo Gallagher, Kwani ligi imekaribia kuanza hivo wanahitaji kupata saini za wachezaji wote ambao wanawahitaji na moja ya mchezaji huyo ni kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga Chelsea.

Acha ujumbe