Kocha mkuu wa Psg, Christophe Galtier amesema kuwa Messi anaweza kuwa mchezaji bora Duniani, kutokana na ubora wake aliouonyesha dhidi ya Nice hapo jana .

 

Galtier: Messi Anaweza Mchezaji Bora Duniani.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina alianza kufunga bao katika ushindi wa 2-1 wa PSG wa Ligue 1 huko Parc des Princes Jumamosi kwa mkwaju wa faulo na  kujishindia mwenyewe. Messi ana mabao matano na assist saba katika mechi mfuluizo za ligi mara ya kwanza akiwa kama mchezaji wa PSG.

Baada ya kupachika mabao katika mechi mfululizo za ligi kwa mara ya kwanza akiwa mchezaji wa PSG, Kocha wa timu huyo Galtier amemuunga mkono mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or.

Galtier: Messi Anaweza Mchezaji Bora Duniani.

“Nina furaha ya ajabu kumuona kila asubuhi mazoezini,” Galtier alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi. “Anacheza vizuri na ana furaha kila siku anapofanya mazoezi”.

Galtier: Messi Anaweza Mchezaji Bora Duniani.

Lakini mshindi wa Kombe la Dunia 2018 Kylian Mbappe aliingia kambani kama kawaida yake na  kuwa ndiye mshindi wa mechi akitokea benchi kwa bao lake la dakika ya 83, na kuipeleka timu hiyo hadi kileleni na kuivuka Marseille.

Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake wa kuanza na Mbappe kwenye benchi baada ya kurejea kutoka Ufaransa, Galtier alisema: “Alipata pigo kwenye nyonga dhidi ya Denmark. Hivyo akawa na muda mchache wa kupumzika na alikuwa na wasiwasi lakini alileta ushindani mkubwa.

Galtier: Messi Anaweza Mchezaji Bora Duniani.

PSG sasa wana pointi 25 baada ya mechi tisa ambazo hawajapoteza hata moja toka  kuanza kwa  kampeni, zinazolingana na mwanzo wao bora zaidi wa msimu wa 2017-18 na 2018-19. Hata hivyo, hazikuwa habari njema kwa wachezaji hao wa Paris, kwani Renato Sanches alidumu kwa dakika 16 pekee baada ya kutolewa benchi, kwa tatizo la majeraha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa