GAMONDI ATUMA UJUMBE MZITO SIMBA

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Yanga, Miguel Gamondi ametuma ujumbe mzito kwa wapinzani wake akibainisha kwamba hawana hofu kuwakabili wapinzani hao uwanjani.

Ipo wazi kuwa Agosti 8 2024 inatarajiwa kuchezwa Kariakoo Dabi katika Ngao ya Jamii ikiwa ni hatua ya nusu fainali, fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 11 kwa mshindi wa mchezo wa Azam FC dhidi ya Coastal Union, itakayochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.Gamondi

Masta Gamondi ameweka wazi kuwa anatambua kuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha wapinzani wao Simba lakini hilo haliwapi tabu kwa kuwa wapo tayari.

“Hatuna ambacho tunahofia kwa wapinzani wetu kwa kuwa tumejiandaa vizuri kiakili na kimwili kuelekea mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa, tupo tayari.

“Tupo imara kiakili na kimwili, tumejianda vya kutosha hakuna tunachohofia, sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani kwani mechi zake nyingi hazikuoneshwa, lakini hiyo sio changamoto kubwa kwani naanda timu yangu kwa asilimia 75, asilimia 25 ndio natumia kumchunguza mpinzani.”

Ipo wazi kuwa msimu wa 2023/24 ni Simba walitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi dhidi ya Yanga kwa penalti 3-1 baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Acha ujumbe