Gareth Bale ameendelea kukaa benchi kwa mechi ya tatu mfululizo katika kikosi cha Zidane. Bale ambaye anaonekana kama anapoteza matumaini na nafasi yake Real Madrid.

Awali alitarajiwa huenda angeondoka pale Real Madrid mapema zaidi, lakini kumekuwa na walakini katika kukamilisha hili. Huku uhamisho wake wa kwenda Uchina ukifeli mara ya mwisho.

Gareth Bale aliwekwa benchi kwa mara ya 3 kwenye mechi dhidi ya Granada. Wiki iliyopita kamera zilimchukua akiwa amevaa barakoa kwenye macho na kujifanya amelala kwenye benchi katika mechi dhidi ya Alves.

Gareth Bale Kuendelea Kuchezea Benchi
Bale akizuga amelala.

 

Kwenye mechi dhidi ya Granada, pia alikuwa akiteneneza mikono yake kama darubini hivi akitazama uwanjani! Mchezo fulani hivi wa kitoto uliovutia zaidi kamera, lakini si dhambi ukifanywa na mtu mzima kama Bale mwenye miaka 30!

Gareth Bale Kuendelea Kuchezea Benchi
Gareth Bale

Wakati akiendelea kuzungumziwa kwa mitazamo tofauti tofauti, wapo wanaodai kuwa bila shaka, Bale ameona kama hazungumziwi sana. Hivyo anatafuta namna ya kuonekana zaidi. Ukizingatia uhalisia kuwa amekuwa katika uhusiano unaotia walakini na meneja Zidane, amekuwa na nafasi ndogo kikosini.

Madrid wanalikaribia zaidi taji la La Liga. Watahitaji ushindi dhidi ya Villarreal ili kujihakikishia wanatwaa taji. Zidane anasema kikosi kwa pamoja kinafikiria namna wanaweza kuliweka taji kibindoni na hawana shida na yale anayoyafanya bale.


 

Kuna ofa kibao sana unzaofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu

Bonyeza HAPA Kujiunga.

40 MAONI

  1. Bale is fadeup being sitting on bench on every match, Its time for Madrid to see what they can for Bale to enjoy football even somewhere else.

  2. Kwa mtazamo wangu zidane ana chuki baina ya wachezaji ingawa haonyeshi kama ana chuki nao kama hamuhitaji amuuze kuliko kudidimiza kipaji chake .

  3. Kiufupi tuu bale si chaguo la zidane mbona iko wazi hilo wala haitaji kutumia nguvu kubwa kufikili ana mchezesha basi tuu kwa sabab hana namna Madrid wenyewe ndio wana mng’ang’ania lakin hayupo kabisa kwenye mipango ya zidane moyo wake ulikua kwa cr7

  4. Duu sio poa kila mechi akae benchi inabidi nae wamfikilie sikila mechi asugue njee sio poa zidane mfikilie kiungo huyo nae apate namba

  5. Zidane amekuwa kama anampotezea bale
    Na anzidi kumsuguliaha benchi inabidi bale aondoke tu akacheze sehemu ingine

  6. Bale nafkiri atakua hana mahusiano mazuri na Zidane kwa uchezaji wa Bale sio mtu wakuwekwa benchi mechi zote,au kama mahusiano ni mazuri na Kocha labda anakua hayupo katika mpango mkakati wake na ni bora aende hata vilabu vya Italia au Uingereza kwani bado ana kiwango kikubwa katika uchezaji.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa