Nahodha wa Wales, Gareth Bale anasema kuwa kwa sasa yuko fiti, na anajiona anazidi kuwa fiti zaidi kila siku.

Katika EURO 2020, Bale anaamini atafanya maajabu zaidi ya aliyoyafanya miezi kadhaa iliyopita. Nyota huyu alishiriki Euro 2016 na kufunga katika kila mechi, anaamini itakuwa zaidi wakati huu.

Katika Euro 2016, Wales walifikia nusu fainali na kutolewa na Portugal. Wales wanaenda kuumana na Switzerland na Bale anaamini ni wakati wa kutamba tena.

Gareth Bale

Nyota huyu wa Real Madrid alifanikiwa kufunga magoli 6 kwenye mechi zake saba za mwisho na Tottenham alikokuwepo kwa mkopo. Akimaliza msimu uliopita kwa magoli 16.

“Najiona niko fiti, vizuri na nina spidi. Nilifunga magoli machache miezi mitatu au minne hivi iliyopita lakini kiwango changu kiliendelea kuwa bora kila mchezo. Nimejitahidi kujiweka sawa, natumaini nitaendelea kuwa hivyo kwenye michuano hii.”

 

Gareth Bale

Gareth Bale akiwa na rekodi ya magoli 33 kwenye mechi 99 za Wales, ana mechi 11 za kimataifa bila kupata goli, huenda hilo likabadilika katika michuano hii ya EURO 2020.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa