Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amekanusha suala ya yeye kuhusishwa na klabu ya Manchester United ambapo yeye ameona sio kitendo cha kiungwana kwasasa.
Kocha Gareth Southgate amesema kuongelea yeye kujiunga na Man United litakua sio jambo la busara na itakua kama kumvunjia heshima kocha wasasa klabuni hapo Erik Ten Hag, Hivo kocha huyo amesema hana cha kuzungumzia zaidi kwenye hilo.Kocha huyo amesema yeye kwasasa ni kocha wa timu ya taifa ya Uingereza na kazi yangu ni kuhakikisha analeta taji michuano ya Euro nchini Uingereza, Huku habari zingine zikiwa sio kipaumbele chake kwasasa.
Kocha huyo amekua anahusishwa sana na klabu ya Manchester United kwa takribani wiki sasa kwa wakati huu ambao kocha Erik Ten Hag ameonekana kutofanya vizuri sana klabuni hapo na kupelekea kuibuka kwa taarifa hizi.Makocha kadhaa wamekua wakihusishwa na kuchukua kibarua cha kocha Erik Ten Hag klabuni hapo, Huku Gareth Southgate akiwa miongoni mwao lakini yeye mwenye amekanusha juu ya kua ni kocha ambaye atachukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo kama Ten Hag ataondolewa kwneye timu hiyo.