Alejandro Garnacho amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na Manchester United. Winga huyo mwenye umri wa miaka 18 siku ya leo aliweka bayana kwenye mkataba wa kumuweka kwenye klabu hiyo ya Ligi kuu ya Uingereza hadi Juni 2028.

Garnacho amecheza mechi 31 kwenye kikosi cha kwanza akiwa na Red Devils na inaonekana kutakuwa na mechi nyingi zaidi zijazo.
Mchezaji huyo wa akademi ya United alisema: “Nilipojiunga na klabu hii ya ajabu, nilikuwa na ndoto ya kufikia mechi yangu ya kwanza, nikicheza Old Trafford, kufunga bao langu la kwanza na kushinda mataji nikiwa na beji hii kifuani. Ninajisikia fahari na kihisia kuwa na uzoefu wakati huu tayari, pamoja na familia yangu ambao wameniunga mkono kila hatua ya njia.”
Sote tumenyenyekea kupata nafasi hii ya kuendelea na safari yetu huko Manchester United na tayari nimeanza kufanya kazi ili kufikia malengo na matamanio yanayofuata. Meneja na wakufunzi wake wamenisaidia kuimarika kwa kila hali, na kwa usaidizi wao, ninaendeleza kila siku kusaidia timu kupata mafanikio. Alisema Garnancho

Kinda huyo amekuwa nje tangu mwezi uliopita kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, lakini anatarajiwa kurejea huku United ikijaribu kutinga hatua ya nne bora na kushinda Kombe la FA.
Mkufunzi wa United Erik ten Hag mnamo Ijumaa alifichua kwamba Garnacho hataruhusiwa kuiwakilisha Argentina watakapoandaa Kombe la Dunia la U20, ambalo litaanza Mei 20.

