Klabu ya Geita Gold inayoshiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika imeanza kwa kupoteza mechi yao ya kwanza wakiwa ugenini dhidi ya Al Hilal Alsahil ya Sudan ambapo Geita walipoteza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa mapema katika kipindi cha kwanza.

 

Geita Gold Yapoteza Ugenini.

Geita Gold ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii baada ya kupanda ligi msimu uliopita na kumaliza katika nafasi ya nne ambayo imemuwezesha yeye kushiriki michuano hii msimu huu huku nyota wa timu hiyo George Mpole akichukua tuzo ya mfungaji bora katika ligi kuu ya NBC akimpiku Fiston Mayele wa Yanga kwa kumpita bao moja. Yeye akiwa na mabao 17, Mayele 16.

Kocha wa timu hiyo Fred Felix Minziro aliiongoza Geita toka ligi daraja la kwanza na hatimaye kupanda nayo ligi na kusajili wachezaji mbalimbali akiwemo Danny Lyanga, Kelvin Yondani, Kelvin Noshan na wengine wengi, ambapo waliweza kuleta ushindani mkubwa kwenye ligi kuu ya Tanzania.  Hadi sasa wanashiriki michuano hii ambapo inakuwa ni kama bahati kwa timu za daraja la katikati kuwa na mwendelezo wa kushiriki michuano hii.

 

Geita Gold Yapoteza Ugenini.

Geita Gold inashiriki michuano hii ya Shirikisho Afrika baada tuu ya kupanda ligi, huku ikiwa ni kama Namungo msimu juzi ambapo nao walipopanda ligi kuu wakafanya vizuri wakashiriki pia kombe la shirikisho ambapo kwa wakati huo walienda kutokana na kufika hatua ya fainali kwenye michuano ya ya Azam sports federation ndipo wakapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo. Wakati huo mechi za Namungo alianza vizuri na ndipo akaanza kupoteza baadae na mojawapo alipoteza mchezo dhidi ya Pyramids ya Misri.

 

Geita Gold na Azam ndio timu mbili pekee zinazoshiriki michuano hii ya shirikisho, ambapo Azam yeye ataanzia raundi ya pili kwenye michuano hii ya shirikisho huku kwa michuano ya Klabu bingwa ikiwakilishwa na Simba na Yanga ambao nao wameanza vizuri michuano hii.

Geita Gold Yapoteza Ugenini.

Sasa ni muda wa Geita kujitafakari na kuangalia wapi walifeli kwenye huo mchezo wa ugenini ili wapate majibu wapi wataanzia, huku nguvu ya ziada ikihitajika zaidi iliwaweze kusonga mbele kwani goli 1 sio mlima marefu wakiwa makini tuu, wanaweza kupindua meza kwenye mchezo ujao.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa