Georginio Wijnaldum anaripotiwa kuwa tayari ameshakubali kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya upande wa Legue 1, Paris Saint-Germain.

Staa huyu anatarajia kukusanya kila kilicho chake klabuni Liverpool baada ya mkataba wake wa sasa kuisha mwezi huu.

Nyota huyu alikuwa anahusishwa na kujiunga na klabu ya Barcelona, baada ya kutajwa kuwa alifanya makubaliano ya awali na Barcelona na ilisalia kukamilisha uhamisho kutimba Camp Nou.

Georginio Wijnaldum Mbioni Kukamilisha Usajili PSG

Lakini kwa mujibu wa The Guardian, Wijnaldum tayari ameshafanya makubaliano na klabu ya PSG, tayari kukamilisha usajili ambao utakamilika mara baada ya kumaliza vipimo vya afya.

Meneja wa PSG, Mauricio Pochettino anaaminiwa kuwa atakuwa amewekeza nguvu ya ziada kushawishi klabu kuinasa saini ya staa huyu. Pochettino ana amini kuwa hiyo ilikuwa fursa adhimu kwa klabu kumsajili mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kama Wijnaldum.

Baada ya kumkosa nyota huyu wa Liverpool, Barcelona wanaaminiwa kuwa sasa wameamua kuhamishia majeshi yao kwa Memphis Depay, ambaye mkataba wake na Lyon unaisha mwisho wa mwezi huu.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa