Siku ya Jumapili staa wa kabumbu kutokea klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hispania, Gerard Pique alisema kuwa yeye bado ana matumaini juu ya fainali za michuano ambayo inadhaminiwa na kampuni yake, Davis Cup na kuwa itaendelea katika jiji la Madrid mwaka huu huu.
Kundi la wawekezaji la Pique, Kosmos lina dili la miaka 25 yenye thamani ya jumla ya dola bilioni 3 baina yake na International Tennis Federation!
Hata hivyo, anaamini kuwa mwezi Novemba kati ya tarehe 23-29 kutakuwa na fainali za kombe hilo nchini Hispania katika mji mkuu wa taifa hilo ingawa kuna balaa la ugonjwa wa Corona kwa sasa.
“Mambo hayatabiriki kabisa, tunajaribu kuwa na uelewa wa kitu ambacho serikali itaamua juu ya michezo yote na endapo tutaweza kuwa na mashabiki ama lah ndani ya Caja Magica,” alisema hayo Pique wakati akiongea na kituo cha televisheni cha Movistar.
“Ninaweza kusema kwamba bado nina matumaini makubwa kwa sababu michuano ya Davis Cup bila ya uwepo wa mashabiki haipendezi kabisa.
“Ninafikiri kuwa hakuna mtu ambaye ana uhakika juu ya yatakayokuja kutokea siku za mbeleni na juu ya kuingia uwanjani tukiwa na mashabiki ama bila ya wao kuwepo. Kadri ambavyo siku zinakwenda mbele ndivyo tunaona ni kwa namna gani tutatambua hali itakavyokuwa kiuhalisia zaidi.”
Hispania, moja ya taifa ambalo limeathiriwa sana na ugonjwa huu, limekuwa na majadiliano juu ya namna ya kulegeza baadhi ya masharti ya kukaa ndani wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa ambao ulianza kushika hatamu tangu katikati ya mwezi wa tatu mwaka huu.
Kuna mipango kuwa wanaotakiwa kuhudhuria endapo kutakuwa na jukwaa la wazi ni watu wapatao 400 pekee na watu 50 endapo watakuwa ndani ya uwanja.
Hispania ilishinda tuzo ya Davis Cup mwaka 2019, walipowapiga Canada 2-0 katika fainali iliyofanyika kule kule mjini Madrid ikiwa ni toleo la kwanza la michuano hiyo iliyoboreshwa zaidi.
Tangu mwezi wa tatu tarehe za katikati kumekuwa na zuio la uendeshaji wa michuano ya tenisi duniani ambapo pia Wimbledon ilifutwa kwa mara ya kwanza kabisa tangu vita vya pili vya dunia viishe na Roland Garros ikahamia mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.
Inatarajiwa kuwa ATP na WTA itarejea tena ifikapo JUlai 13 mwaka huu endapo mambo yakiwa sawa kiafya.


hamidu
sante kwa taarifa vzr. mmoja wa mabeki bora wazuri.#meridianbettz
Theckla
Mungu aepushe tu hili janga la corona na pique matumaini yake yatakuwa sahihi
Tatu
Nashukulu kwa taarifa
mathayo sonje
daah!!! kumbe pique sio mpila tuu, hata tennis yupo, safi sana
Lombo
meridianbet hamjawai kuboa
Povel
Asante meridian kwa habar Moto Moto za Kimichezo meridian bet tz#
Gabriel
Good news 👍@ meridianBetTZ
winfrida
gerard yuko vzr namkubali uyu beki
Ernest
Well said Gerard Pique.
felister
asanteni kwa taarifa nzuri meridian
Shafii
Itakua imekaa poa kwa Gerard
khadija
ahsante kea taarifa meridian nawakubali sana
Ester mmakasa
Ni taarifa nzuri tunashukuru meridianbet kutujulisha.
Aziza mushi
Meridiani mpo vizuri hamchelewi kutupa taarifa watu wenu asanteni👏
Frank patrick
Aisee ni michezo yote bila mashabiki hainogi kabisaa
Antony Luseno
Nice #meridianbettz
mariam mtandama
meridianbet mko juu #meridianbettz
Theonestina
Asante meridianbet kwa taarifa
Furahav
Itakuwa poa.
farida ahmadi
Gerrad pique alikuwa beki bora San nadani ya klabu ya Barcelona pia habari nzuri meridianbettz Asante kwa taarifa