Ghana Mpaka Premier League…

Yeboah? Gyan? Essien? Unadhani ni nani kati ya hao wachezaji waliotokea nchini Ghana walikuwa mahiri walipochezea ligi ya Uingereza nyakati zao?

Leo tupo upande wa Afrika ya Magharibi kutazama vipaji lukuki ambavyo vilikwenda kufanya vyema sana ndani ya ligi kuu ya nchini Uingereza na kuweza kuweka historia za namna yake ndani ya mashindano hayo.

Tnnawafurahia na kusherehekea mafanikio yao kisoka walipokuwa Ulaya.

Hapa ni kwa upande wa taifa la Ghana ambapo jumla ya wanasoka 25 wameiwakilisha vyema sana Afrika Magharibi hususan taifa la Ghana katika michuano ya Uingereza. Kwanza kabisa Nii Lamptey aliichezea klabu ya soka ya Aston Villa mwezi wa Septemba mwaka 1994.

Tony Yeboah alikuwa ndiye mfungaji wa kwanza kabisa kutokea Ghana katika mashindano hayo pale alipoifungia klabu yake ya Leeds United mwezi Februari mwaka 1995.

Ilikuwa ni goli mojawapo kati ya yale 24 aliyoyafunga akiwa Premier League ambapo mengine yalikuwa yanavutia mno.

Unaweza kutazama magoli maridadi kabisa kutoka kwa washambuliaji kama akina Ayew na kaka yake, Michael Essien pamoja na Tony Yeboah.

Kwa hakika, takwimu za magoli kwa mchezaji Yeboah yanawazidi wenzake wa taifa moja hata wakiungana ingawa anakaribiwa sana na Jordan Ayew.

Fowadi wa klabu ya soka ya Crystal Palace amefunga mabao nane katika kazi yake ya kucheza soka mpaka sasa katika msimu huu, anajivunia kuwa na magoli yapatayo 24 tangu ajiunge kwa mara ya kwanza akiwa na Aston Villa wakicheza dhidi ya upande wa Swansea City ambako kulikuwa na kaka yake aitwaye, Andre Ayew.

Tukiongelea kucheza mechi nyingi zaidi uwanjani huyu bwana Michael Essien anaongoza njia akiwa na jumla ya mechi 168 alizocheza kwa ajili ya klabu ya soka ya Chelsea. Bingwa huyo mara mbili ni mmoja kati ya Waghana watatu pekee waliofanikiwa kunyanyua taji la ligi kuu ya Uingereza, Premier League.

Wengineo akina Jeffrey Schlupp na mwingine Daniel Amartey, wote walikuwa ni sehemu ya historia kubwa ya klabu ya soka ya Leicester City kunyanyua taji la msimu wa 2015/16.

Takwimu zinazoongoza kwa Waghana ndani ya PL

MechiMagoliAssists
Michael Essien168Tony Yeboah24Michael Essien10
Jeffrey Schlupp143Jordan Ayew24Andre Ayew9
Jordan Ayew128Andre Ayew21Jordan Ayew8
John Pantsil94Michael Essien17Jeffrey Schlupp7
Andre Ayew89Asamoah Gyan10Christian Atsu6
Christian Atsu79Jeffrey Schlupp10Sulley Muntari5

 

Kepteni anayeongoza kwa taifa la Ghana ambaye pia ni mfungaji bora zaidi wa magoli alifanikiwa pia kuacha alama yake kwenye michuano ya Premier League.

Wakati Asamoah Gyan akihudumu katika mashindano hayo alifikia jumla ya mabao 10 katika msimu mmoja pekee akiwa na klabu ya soka ya Sunderland, ambapo aliungana na mwenzake kwa mkopo, Sulley Muntari.

Misimu mitatu kabla ya mchezaji Muntari hajaisaidia klabu ya Portsmouth kufikia mafanikio yao makubwa ya juu zaidi ndani ya Premier League msimu wa mwaka 2007/08 wakimaliza katika nafasi ya nane na akashinda taji la FA Cup.

Unaweza kutazama magoli bora sana kutoka kwa wachezaji wakubwa wa taifa la Ghana na kutazama takwimu za hapo juu na kuona namna ambavyo wamechangia katika mafanikio ya soka la Ligi Kuu ya Uingereza, Premier League na ni kwa wachezaji bora kabisa wa kutoka taifa la Ghana.

Tuambie neno hapo. Ni nani miongoni mwa hawa alifanya vyema akiwa Premier League wakitoka katika taifa la Ghana?

  • Jordan Ayew
  • Michael Essien
  • Asamoah Gyan
  • Sulley Muntari
  • Tony Yeboah

25 Komentara

    Michael essien ndie mghana aliyenivutia ukiondoa hao wote

    Jibu

    Kwangu mimi kiungo Michael Essien namupa heko kwa mchango mkubwa alitoa kwenye timu yake ktk EPL. Hakuwa mfungaji bali alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea

    Jibu

    Hapo Michael Essien. .mpo vzr kwa habari za michezo.

    Jibu

    Yeboah ndo naona alikuwa bora zaidi

    Jibu

    Wote walikuwa Bora sanaa wakiwa uwanjani

    Jibu

    100% Michael Essien was the best

    Jibu

    Essien ndio baba lao

    Jibu

    Essien yuko poa amefanya maajabu sana baran ulaya ata Africa timu yake ya taifa

    Jibu

    Wote walikua vizuri uwanjan

    Jibu

    Michael essien kiungo Bora Sana

    Jibu

    Essien alikua bora

    Jibu

    Wote walikuwa wakali

    Jibu

    Hapo naona wote wako vizuri

    Jibu

    Tony yeboah namkubali sana ni mchezaji mahiri sana kutoka ghana safi sana kwa hatua waliofikia ghana asanten meridian kwa taarifa za kimichezo

    Jibu

    Michael Essien yupo vizuri zaidi

    Jibu

    Yeboah alikua hatar sana

    Jibu

    Aaah michael Essien katishaa yuko vzr

    Jibu

    Tony Yeboah huyu ni mkongwe anaeishi kwenye soka alikua mkali sana #meridianbettz

    Jibu

    Michael essien namkubali sana

    Jibu

    Wote wakali bhana

    Jibu

    Ghana wamechukua hatua nzuri

    Jibu

    Essein alitisha

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa#meridianbet

    Jibu

    Tony Yeboah mtu mbaya sanaaaaaa

    Jibu

    Mna makala nzur sana meridianbet

    Jibu

Acha ujumbe