Gianluigi Donnarumma Rasmi PSG Miaka 5

Mlinda mlango wa Italia Gianluigi Donnarumma amesaini mkataba wa miaka mitano na
Paris St Germain.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anajiunga na PSG baada ya kumaliza mkataba wake na AC Milan, ambao alikuwa nao tangu 2013.

Donnarumma alipewa mkataba wake wa kwanza wa Milan akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2015 na akaishia kucheza zaidi ya 200 za Serie A.

Gianluigi Donnarumma Rasmi PSG Miaka 5

Uthibitisho wa kuhamia kwake PSG unakuja siku tatu Donnarumma akitoka kuisaidia Italia kushinda Euro 2020 na kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Donnarumma alisema katika nukuu kwenye tovuti rasmi ya PSG kuwa: “Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya klabu hii kubwa ambayo ni Paris St Germain.

“Ninahisi nipo tayari kubeba changamoto hii mpya, na kuendelea kukua hapa. Nikiwa na Paris, ninataka kushinda mara nyingi iwezekanavyo na kuwapa furaha mashabiki.”


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe