Miongoni mwa wamiliki wa klabu ya Manchester United Avram Glazer amemtakia kila la kheri gwiji wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo ambae ameondoka klabuni hapo siku kadhaa zilizopita.

Klabu ya Manchester United ilitoa taarifa siku tatu zilizopita kua wamekubaliana na mchezaji huyo kuvunja mkataba wake kabla ya kumalizika kwa muda na nyota huyo atatafuta timu punde tu baada ya michuano ya kombe la dunia.glazerBwana Glazer yeye alipopata nafasi ya kuulizwa kuhusu nyota huyo ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa vipindi viwili tofauti akasema “Ni mchezaji mkubwa aliyewahi kuitumikia Manchester United, Naheshimu kila alichokifanya kwa klabu hii na namtakia kila la kheri”

Nyota huyo ambaye ameondoka klabuni hapo kwasababu ya kutokuelewana na kocha pamoja na uongozi wa timu hiyo kwenye baadhi ya mambo huku mahojiano aliyoyafanya na mwandishi nguli Piers Morgan siku kadhaa yakichochea zaidi kuondoka kwake.glazerPia familia ya Glazer ipo mbioni kuiuza klabu ya Manchester United ambapo wameiweka sokoni mpaka sasa huku ikielezwa sababu kubwa ni mahojiano ya Ronaldo ambayo yaliweka kila kitu wazi, Huku akiseleza namna wamiliki hao wanaiendesha timu vibaya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa