Gnabry Apata Majeraha Kwenye Fainali Dhidi ya Tigres.

Serge Gnabry anajiandaa kukaa nje ya dimba baada ya kupata jeraha la misuli katika paja lake la mguu wa kushoto Bayern Munich yathibitisha.

Gnabry Apata Majeraha Kwenye Fainali Dhidi ya Tigres.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alitolewa nje dakika ya 64 ya mchezo katika fainali ya Club World Cup ambapo Bayern Munich iliibuka na ushindi wa 1-0 na kuwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.

Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich hawajaweka wazi ni kwa muda gani mchezaji huyo wa miaka 25 atakaa nje ya dimba ambapo pia walikuwa bila Thomas Muller ambaye alikutwa na maambukizi ya Coronavirus jijini Qatar.

Taarifa rasmi ya klabu ilisomeka: “Kwa muda uliyopo Bayern watakuwa bila Serge Gnabry.

“Mshambuliaji amepata jeraha la misuli katika paja lake la mguu wakushoto siku ya jana katika fainali ya Club World Cup dhidi ya Tigres. Haya yalikuwa na majibu ya vipimo viliyofanywa na idara ya matibabu ya Bayern Munich.

Baada ya kushinda Club World Cup, Bayern watarudi dimbani kuchuana na Arminia Bielefeld siku ya Jumatatu wakiwa nyumbani mchezo wa Bundesliga.

Kisha watacheza dhidi ya Lazio katika michuano ya Champions League hatua ya 16 bora Februari 23 harafu watawakabili Borussia Dortmund mwezi March.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

11 Komentara

    Pole Sana ndo changamoto za kazi

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Bayern inamuhitaji sana Gnabry kwasasa kuliko wakati mwingine wowote kutokana na kukabiliwa na majeruhi ktk nafasi muhimu

    Jibu

    Pole gnabry

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Majeraha sio poa kabisa

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Bayarn imekabiliwa sana na mejeruhi tena wote wamuhimu

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole kwako

    Jibu

    pole yake

    Jibu

Acha ujumbe