Gomes : Tupo Tayari Kuwavaa AS Vita


Kocha wa Simba, Didier Gomes amesisitiza kwamba sasa akili zao wameelekeza DR Congo kwenye mechi dhidi ya AS Vita hii na lazima wafanye kitu.

β€œTunatambua tunaenda kukutana na timu kubwa ambayo shauku yake ni kushinda mechi ya kwanza ya hatua ya makundi kama ilivyo kwetu, tunajiamini na wachezaji wangu wote wapo kwenye ari nzuri ya ushindani na tupo tayari kwa mapambano.

 

β€œMashindano ya Simba Super Cup yalitupa mwanga wa wapi pa kuanzia, ukiangalia kwenye michezo yetu minne iliyopita dhidi ya Al Hilal, TP Mazembe, Dodoma Jiji na Azam tumeongoza kwa kutengeneza nafasi za mabao kuliko timu yeyote ile hivyo hicho ni kiashiria kuwa tunaweza kupata matokeo chanya mbele ya timu yeyote ile,”

alisema Gomes ambaye ana uzoefu na mechi za Afrika akiingoza El Merreikh ya Sudan kuwazuia Enyimba ya Nigeria kutinga makundi ya Afrika nyumbani kwao.

β€œNi kweli mechi dhidi ya Azam wachezaji wamekosa mabao mengi ya wazi lakini hicho sio kigezo cha kuwabeza, kuwaadhibu ama kusema sio bora kwani hayo mambo yanatokea kwenye soka kikubwa ni kuendelea kuyafanyia kazi makosa yale ili yasiwe yanajirudia mara kwa mara,” aliongeza Gomes.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBETΒ 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenyeΒ  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

11 Komentara

    Naamini simba watafanya vizuri

    Jibu

    Simba hawashindwi

    Jibu

    Simba wamejipanga Sana na wapo tayari kuwakabiri kivyovyote

    Jibu

    Utakuwa mchezo mgumu hasa ikizingatiwa walishaifunga Simba bao 5 mwaka 2019.

    Jibu

    Simba watawaweza kweli AS vita au maneno tu

    Jibu

    Mchezo huo atutauwachia Wana Simba lazima tukaze

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Vita 5 simba 0

    Jibu

    Tunasubiri tuone

    Jibu

    Kaz kaz

    Jibu

    Simba round hii wanajiamini sana

    Jibu

Acha ujumbe