Kocha mpya wa Chelsea Graham Potter amefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika klabu hiyo baada ya kuifunga klabu ya Crystal palace kwa jumla ya goli mbili kwa moja.

graham potterkocha huyo amechukua nafasi ya mjerumani Thomas Tuchel klabuni hapo ameingia uwanjani kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa pili huku ikiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza na kufanikiwa kupata alama tatu.

Ni Crystal Palace waliofanikiwa kupata bao la mapema kupitia kwa Edourd kabla ya Aubameyang kusawazisha na timu hizo kwenda mapumziko wakiwa wamefungana bao moja kwa moja.

Kipindi cha pili Vijana wa Graham Potter walikuja wakiwa na ari ya juu na kuonesha wanataka ushindi katika mchezo huo baada ya kukosa nafasi mara kadhaa hatimae wakafanikiwa kupata goli kupitia kwa mchezaji Conor Gallagher dakika ya 90 ya mchezo na kupelekea Chelsea kupata alama tatu muhimu.

graham potterGraham Potter ambae amefanya vizuri katika klabu ya Brighton anatazamiwa kufanya makubwa klabuni hpo huku bosi wa klabu hiyo Toed Boehly akidai kocha huyo kaletwa klabuni hapo kwa mipango ya muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa