Mchezaji wa Manchester City Jack Grealish ameshangazwa na “tatizo” la Graeme Souness baada ya nahodha huyo wa zamani wa Liverpool  kukosoa uchezaji wake Manchester City.

 

Grealish Ashangazwa na Ukosoaji wa Graeme Juu Yake

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza Jack Grealish alijiunga na City kwa uhamisho uliovunja rekodi ya Uingereza kwa Pauni milioni 100 mwaka 2021 lakini amekuwa na wakati mgumu kufikia kiwango alichokuwa nacho akiwa Aston Villa.

Baada ya ,mabao 6 na assist 10 katika mechi 26 za Primia ligi kwa Villa mnamo 2020/21, Grealish alichangia mabao matatu pekee na assist tatu katika idadi sawa ya mechi katika kampeni yake ya kwanza ya Manchester City.

Ameanza msimu wa 2022/23 polepole pia, ingawa winga huyo wa Uingereza alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Wolves siku ya Jumamosi ambapo Souness alisema Grealish;

“Si mchezaji mzuri”, anachukua miguzo mingi sana” na “hatoi vya kutosha” ukosoaji ambao uwewaacha City wakishangaa.

 

Grealish Ashangazwa na Ukosoaji wa Graeme Juu Yake

“Sijui shida yake ni nini ; huwa anasema kitu kunihusu, lakini najaribu kutoisoma sana,” Grealish alisema

Aliendelea kusema kuwa Souness alikuwa mchezaji mzuri na alishinda mengi lakini hajui kile anachoongea kumuhusu yeye Grealish anajua uwezo wake yeye mwenyewe na pia anajua hapo awali ambapo mchezaji huyo wa zamani wa Liver alikuwa akisema kuhusu yeye kutosogeza mpira kwa haraka lakini anapocheza na meneja kama Guardiola anafata maelekezo yake.

“Siku zote nitawafanya watu wazungumze kama sichezi vizuri.Huwa natazama mechi zangu nyuma, na ninajilaumu sana. Najua kulikuwa na michezo hasa katika kipindi cha pili cha msimu uliopita ambapo sikuwa bora wakati wote”.

 

Grealish Ashangazwa na Ukosoaji wa Graeme Juu Yake

“Nilirudi nikiwa fiti na nilirudi nikiwa na maandalizi mazuri lakini niliumia kwenye mchezo wa pili, na ndiyo maana nasema kuanzia sasa naenda kuinamisha kichwa chini na kujaribu kurejesha utimamu huo, kwasababu najua kwamba bado sijafika asilimia 100 .

Grealish ni sehemu ya kikosi cha England kwaajili ya michezo ijayo ya Ligi ya Mataifa dhidi ya Italia na Ujerumani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa