Meneja wa Manchester United Ole Gunnar anasema nyota kinda wa klabu hiyo Mason Greenwood amepikika tayari. Sasa anaweza kuichezea timu ya taifa ya Uingereza.

Kinda huyu mwenye miaka 18 tu amekuwa kwenye fomu nzuri pale Old Traford. Ole Gunnara ana uhakika kuwa nyota huyu anaweza kufanya vyema ikiwa ataitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa cha Uingereza.

Greenwood amekuwa akifananishwa na nyota wa zamani wa Man United Robin van Persie. Mpaka sasa amewafungia United jumla ya magoli 15 kwenye michuano yote, 8 yakiwa ni ya Ligi ya Primia.

Greenwood  Anafaa kwa Uingereza Sasa
Mason Greenwood

Greenwood aliona lango mara mbili kwenye mechi dhidi ya Bournemouth ambao wanakalia kuti la moto, karibu na kushuka daraja. United waliwafunga jumla ya bao 5-2.

Solskjaer anaamini huu ni wakati wa Gareth Southgate kumuita kinda huyu kikosini, na bila shaka atafanya maajabu katika kikosi hicho.

Imani ya meneja Solskjaer  ni kuwa kama umeweza kuichezea Man United basi unaweza kuichezea timu yeyote.

“Ukiichezea Man United nafikiri ni jaribio zuri na gumu kutosha kuchezea timu nyingine yeyote. Ukiiweza mikiki mikiki ya kuchezea Man United basi unaweza kuichezea timu yeyote na Mason anao huo ubora ambao wengi hawana. Hivyo anaweza kuwa kwenye kikosi cha U21 cha Uingereza bila shaka. Anacheza vizuri kwetu.” -Ole Gunnar Solskjaer

 


Unajua kuwa Meridianbet wanatoa mizunguko 50 ya bure kwa mteja mpya? Jisajili sasa na ufurahie burudani na ushindi wa Kasino ya Mtandaoni.

JISAJILI HAPA

Mizunguko ya Bure | Kasino ya Mtandaoni

 

50 MAONI

  1. Huyu dogo ni hatari sana na anaweza kabisa kuichezea timu take ya taifa na atafanya vizuri na kuweka Record kubwa na ya England

  2. Ni kweli yupo sahihi kwa wachezaji makinda Kama hawa wanapo parfom vizuri ndio wakati wao wa kuwapa nafasi ya kucheza zaidi ili waweze kujijengea uzoefu Mara dufu.

  3. Ni.habar njema kwa timu ya taifa ya uingereza kwa ujio na kiwango cha juu kinda huyu kwa sasa anacho onesha ana uwezo mkubwa na kukwamiaha mpira wavuni kila anapopata nafasi ya kufunga

  4. Kweli yupo sahii kwa wachezaji makinda Kama hao wanapo parfom vizuri ndio wakati waho wakuwapa nafasi kucheza zaidi

  5. Greenwood yupo poa sana licha ya kufanianishwa na nyota wa uholanzi aliyejipiga man United Robin van persie Ila kuna vitu kama anavyokimbia na matege yake pia anavyopiga miguu yote yote kama van persie vile vile dogo yupo poa sana

  6. Greenwood ni vizuri kama wamempa nafasi kwa uingereza kwasababu ni kinda anaejituma na ana uwezo wa kufikiri haraka sana .

  7. yp yupo vizur na anastahili kabisa kubaki uengereza coz anafqnya vzr sana pale mashetan wekundu( manchester) na anamchango mzur sana pale kilabuni…

  8. Greenwood ameiva sana ole amejua kumchezesha na kumpa kujiamini uwanjani na hiyo imemfanya awe imara kwa mda mfupi kiasi mashabiki kumfananisha na vanpersie

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa