Greenwood Atolewa Kwa Mdhamana.

Joto bado ni kali kwa Mason Greenwood wiki hii. Mikono ya sheria inaendelea kumshikia toka wikiendi iliyopita.

Greenwood anashikiliwa na polisi wa jiji la Manchester kwa mahojiano na uchunguzi wa vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake. Hii ni baada ya mpenzi wake kuweka video na ushahidi wa sauti unaosadikika kuwa Mason ndio muhusika wa shambulizi lililompata binti huyo.

Wakati akiwa anashikiliwa kwa tuhuma hizo, Jumanne hii amekutwa na tuhuma zingine zinazohusishwa na ubakaji pamoja na tishio la kuua. Ama hakika, Mason anawakati mgumu.

Akiwa ni kijana mdogo wa miaka 20, Greenwood anapitia kipindi kigumu nje ya uwanja. Baadhi ya wachezaji wenzake wanasadikika kumuondoa kwenye orodha za wafuasi wao kupitia mitandao ya kijamii.

Wakati hili likiwa linaendelea, Manchester United wametoa tamko la kupinga vikali vitendo vyote vinavyohusiana na ukatili. Vilevile, Mason hatorejea kwenye mazoezi wala kuitumikia timu hiyo mpaka pale itakapotaarifwa zaidi.

Mbali na United, Nike ambao ni washirika wa Mason, wametangaza kusitisha ushirika na mchezaji huyo mpaka pale watakapotoa taarifa nyingine. Zote zikiwa ni jitihada za kuonesha kutopendezwa na kinachoendelea kumuhusu mchezaji huyo.

Japokuwa hakuna taarifa wala tamko lolote lililotolewa na Mason au mtu yeyote wa karibu na mchezaji huyo, taarifa iliyotoka hivi punde ni kuwa, mchezaji huyo ametolewa kwenye kituo cha polisi kwa mdhamana wakati uchunguzi na mahojiano zaidi yakiendelea.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe