Winga wa klabu ya Manchester United na raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Greenwood inaelezwa huenda akaendelea kukipiga ndani ya klabu ya Getafe kwa mwaka mwingine.
Ameyazungumza hayo rais wa klabu ya Getafe Angel Torres amesema mchezaji huyo anaweza kusalia ndani ya klabu hiyo msimu ujao, Licha ya kwamba mchezaji huyo anatakiwa kuuzwa na klabu yake ya Manchester United.Rais Angel Torres amekanusha taarifa za Greenwood kutakiwa na klabu ya Atletico Madrid huku akisema klabu pekee ambayo ilikua na mpango na mchezaji huyo ni Barcelona ambao kwasasa ameeleza kua sio kipaumbele chao tena.
Klabu ya Manchester United ina mpango wa kumuuza winga huyo katika dirisha kubwa lijalo kwa dau zuri, Jambo hilo linamfanya Angel Torres kuamini kama klabu zitashindwa kulipa dau zuri wao wanaweza kupata fursa ya kuendelea kumtumia kwa mkopo kwa mwaka mwingine.Winga Mason Greenwood amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Getafe jambo ambalo limefanya klabu hiyo kutaka kuendelea kubaki nae msimu ujao, Lakini Man United imedhamiria kumuuza katika dirisha kubwa linalofata mwezi Julai.