Greenwood Kubaki United?

Winga wa Manchester United ambaye alikua kwa mkopo klabu ya Getafe ya nchini Hispania Mason Greenwood amejumuishwa kwenye kikosi kitakachobaki ndani ya klabu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Swali kubwa ni kua je winga Greenwood atabakia ndani ya kikosi cha Man United baada ya kujumuishwa kwenye kikosi chao cha msimu ujao?Kwani kuna taarifa mbalimbali ambazo zinaeleza kua mchezaji huyo ana nafasi kubwa ya kuuzwa ndani ya timu hiyo.greenwoodSwali hili limekuja baada ya wachezaji ambao klabu hiyo haina mpango nao kumalizana nao mapema na kuwaaga, Japo inaelezwa bado klabu hiyo inafikiria kumuuza mchezaji huyo lakini tu kama watapata klabu ambayo itatoa ofa nzuri.

Wachezaji wengine ambao wameorodheshwa kwenye kikosi cha Man United msimu ujao na mashabiki wengi wa United wakionekana kutoridhishwa ni wachezaji kama Harry Maguire, Scott Mctominay pamoja na winga Antony Santos.greenwoodPamoja na wachezaji kama Mason Greenwood kujumuishwa kwenye kikosi cha msimu ujao cha Man United na kuibua hisia kwa mashabiki wa klabu hiyo huenda mchezaji akasalia klabuni hapo, Lakini ukweli ni kua pamoja na kujumuishwa kwake lakini ofa nzuri ikija kama taarifa zinavyoeleza atauzwa kwenda sehemu nyingine.

Acha ujumbe