Mshambuliaji kinda wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood amejitoa kwenye kikosi cha Uingereza kinachojiandaa na michuano ya EURO 2020 baada ya kupata majeraha yatakayomuweka nje kwa muda.
Ripoti rasmi kutoka Manchester United zinasema kuwa Greenwood alikuwa na majeraha toka mwezi machi lakini alichezeshwa mechi kwa uangalizi maalum na hivyo kama timu haioni umuhimu wa Mchezaji huyo kushiriki mashindano hayo na hivyo atalazimika kubaki United ili aweze kupona majeraha.
Greenwood amekuwa na wakati mzuri na Manchester United akiwa na umri wa miaka 19 tu amecheza michezo 105 na kufunga magoli 29. Msimu huu Greenwood ameonesha ujuzi wake kwa msimu huu tu amecheza mechi 31 na kufunga magoli 7 huku akitoa asisti 2.
Utimamu wa mchezaji huyu ni muhimu sana kwenye kikosi cha Manchester United na hii ndio sababu United wametangaza rasmi mchezaji huyo apone kwanza majeraha yanayomsumbua.
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Pole yake
Pole yake
Pole sana