Gremio Yamsajili Mshambuliaji wa Uruguay Suarez

Luis Suarez amejiunga na klabu ya Gremio ya Brazil kwa mkataba wa miaka miwili. Mshambuliaji huyo wa Uruguay alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka katika klabu yake ya utotoni Nacional na ataendelea na soka lake nchini Brazil.

 

Gremio Yamsajili Mshambuliaji wa Uruguay Suarez

Suarez alitakiwa na timu ya Mexico Cruz Azul, lakini Gremio wameshinda kinyang’anyiro cha kuwania saini yake. Klabu ya Gremio yenye maskani yake Porto Alegre ilithibitisha kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 katika mkesha wa mwaka mpya.

Suarez aliisaidia Nacional kushinda taji la Ligi Daraja la Kwanza baada ya kurejea katika nchi yake baada ya kuondoka Atletico Madrid.

Gremio Yamsajili Mshambuliaji wa Uruguay Suarez

Mkongwe huyo alishinda mataji manne ya LaLiga katika kipindi cha mafanikio makubwa akiwa na Barcelona na kutwaa jingine akiwa na Atletico katika kampeni za 2020-21.

Pia alinyanyua taji la Ligi ya Mabingwa akiwa Barca mnamo 2015.

Suarez alishinda Copa America akiwa na Uruguay mwaka wa 2011, na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa nchi yake, akiwa na mabao 68 katika michezo 137, ingawa alishindwa kufunga wakati wa kampeni zao za hivi majuzi za Kombe la Dunia huko Qatar 2022.

Gremio Yamsajili Mshambuliaji wa Uruguay Suarez

Acha ujumbe