Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemkingia kifua kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza Kalvin Phillips ambaye anaonekana ameanza kwa kusuasua klabuni hapo.
Kocha Guardiola ambaye alisema wiki kadhaa nyuma kua mchezaji huyo alirudi kutoka kwenye michuano ya kombe la dunia akiwa ameongezeka uzito kupita kiasi, Na kumtaka kiungo huyo kufanya mazoezi kwa bidii ili kuweza kurudisha mwili wake ili kuonesha makali zaidi.Kumekua na maneno mengi juu ya kiungo huyo aliyetoka klabu ya Leeds majira ya joto akijiunga na Manchester City amekua akipokea maneno ya mashabiki wakiamini kua klabu hiyo imesajili mchezaji wa kiwango cha chini, Lakini kocha wake Pep Guardiola amesisitiza mchezaji wake huyo atakua sawa siku za hivi karibuni.
Kocha huyo amesema kua kiungo huyo anahitaji muda kidogo kwajili ya kuweza kua fiti na kuonesha ubora mkubwa ndani ya klabu hiyo, Hivo watu wasimpe presha kiungo huyo ambaye anatarajiwa kuanza mchezo wake wa kwanza kesho kwenye kombe la Carabao dhidi ya klabu ya Southampton.Klabu ya Man City chini ya kocha Pep Guardiola itakua na mchezo wa kombe la Carabao kesho hatua ya Robobo fainali ya michuano hiyo. Huku kiungo Kalvin Phillips akitarajiwa kuanza kwa mara ya kwanza katika mchezo huo akiwa na jezi ya klabu hiyo.