Guardiola Amtabiria Makubwa Thomas Frank

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemtabiria makubwa kocha wa klabu ya Brentford Thomas Frank na kusema ni suala la muda tu kocha huyo atajiunga na moja ya vilabu vikubwa barani ulaya.

Guardiola anamuona  Thomas Frank kama kocha ambaye anastahili kukaa kwenye benchi la moja timu kubwa barani ulaya, Kwani amesema anaona uwezo wa kocha huyo ni mkubwa sana kwa kauli hiyo ni wazi kocha huyo wa Man City anaona Thomas Frank hastahili kubaki ndani ya Brentford kwa muda mrefu.

“Ni suala la muda tu kabla ya Thomas Frank kujiunga na klabu kubwa ya Ulaya. Ataipata.”

“Watachukua kocha mzuri, na hilo litatokea.”

“Nina uwezo katika mambo machache, lakini kusoma kocha mzuri, najua ni yupi mzuri…”

Kocha Guardiola aliyazungumza hayo baada ya mchezo wao kumalizika dhidi ya Brentford ambao wanafundishwa na kocha Thomas Frank, Mchezo ulionekana kua mgumu sana kwa Man City na mara kadhaa City wamekua wakiteseka wakikutana na Brentford ambapo inaweza kua moja ya sababu ya Pep kummwagia sifa Thomas Frank.

Acha ujumbe