Guardiola Anaamini Foden Atarudi Kwenye Ubora Wake

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kua anaamini mchezaji wake Phil Foden atarejea kwenye ubora wake baada ya kua na kiwango cha chini baada ya kutoka kwenye michuano ya kombe la dunia.

Kocha Pep Guardiola anaelewa fika tangu Phil Foden ametoka kwenye michuano ya kombe la dunia hajarudi kwenye ubora wake, Lakini kocha huyo anaamini mchezaji wake huyo atarejea kwenye ubora wake ambao amekua nao kwa mudamrefu ndani ya timu hiyo.guardiolaKiungo Phil Foden amekua akisumbuliwa na majeraha ya enka tangu amerejea ndani ya klabu hiyo akitokea kwenye michuano ya kombe la dunia, Huku ikitajwa kua moja ya sababu zinazomfanya mchezaji huyo kutokua kwenye ubora wake.

Kocha Guardiola amefichua kua pia kiungo Phil Foden alimfata na kumuomba mapumziko baada ya kuona hawezi kucheza, Hivo kocha huyo na uongozi wake kwa ujumla waliamua kumpa mapumziko ili kumsaidia mchezaji huyo aweze kurejea kwenye ubora wake.guardiolaPamoja na kiwango kikubwa cha Riyad Mahrez kwasasa pamoja na mchezaji Jack Grealish ambaye anaonekana kuimarika zaidi msimu huu, Lakini kocha Guardiola amesisitiza kua Foden ni almasi kwao ni amepoteza kujiamini tu kwasasa lakini anaamini mchezaji huyo atarejea.

Acha ujumbe