Suala la hatma ya Lionel Messi bado ni gumzo kwenye vyanzo mbalimbali vya habari za michezo. Guardiola ni moja ya mameneja wanaomkubali sana Messi, huku safari ya Messi kutua Premier League ikipigwa upatu zaidi.

Meneja wa Man City, Pep Guardiola tayari amesaini mkataba wa kuendelea kuwepo Manchester City kwa miaka miwili zaidi. Ni matarajio ya watu wengi kuwa sasa uhamisho wa Lionel Messi kuingia Man City utakuwa na nafasi nzuri zaidi.

Msimu wa joto, Man City walijaribu kufanya mipango ya saini ya Lionel Messi wakati staa huyu alipoweka wazi alitaka kuondoka Barcelona. Suala hilo halikuwezekana kwa kuwa Barca walimlazimisha abaki.

Barcelona wanatarajia kuendelea kumshawishi Messi kusalia, ambaye mpaka sasa hajabainisha msimamo wake rasmi.

Kufuatia kusaini dili jipya, Guardiola anaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuinasa saini yake, na anatarajiwa huenda akakutana na Messi kwa mara nyingine.

Guardiola Angependa Messi Asalie Barcelona
Guardiola tayari alifanya kazi na Messi Barcelona. Anaamini ni heri Messi asalie huko.

Hata hivyo, kwa Upande wa meneja huyu wa City, yeye anasema kama mpenzi wa Barcelona, angetamani nyota huyo Asalie Barcelona.

Guardiola alinukuliwa akisema;

” Ni mchezaji wa Barcelona, kama ukiniuliza maoni yangu, ninaheshimu sana Barcelona walichonifanyia kama mchezaji na kama meneja. Walinipa kila kitu, ninachopenda amalize soka lake akiwa Barcelona.”

“Nimesema mara elfu moja, kama shabiki wa Barca, hicho ndiyo ninachopenda. Lakini ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake sijui nini kitatokea.”

Ikiwa Messi atakuwa na msimamo wa kuondoka Barca, klabu anazohusishwa nazo zaidi ni Man City, Inter Milan na PSG.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

 

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa