Guardiola Asema United imerudi Kwenye Ubora

Kuelekea mchezo wa Derby kati ya Manchester United na Manchester City kocha Pep Guardiola amesema anaiona klabu ya Manchester United imerudi kwenye ubora wake.

Kocha Guardiola amezungumza kuelekea mchezo unaovitunisha vilabu hivo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mapema leo katika dimba la Old Trafford. Kocha huyo amesema klabu hiyo imeanza kuonesha ubora siku za hizi karibuni ambao ilikua nao siku za nyuma.GuardiolaKlabu ya Man United imefanikiwa kushinda michezo sita mfululizo katika michezo yao sita ya mwisho ambapo wamefanikiwa kuruhusu goli moja pekee kwenye michezo hiyo, Hii inaonesha namna ambavyo klabu hiyo imeimarika siku hizi za karibuni.

Pep Guardiola amesema ” Nimeshasema mwezi mmoja au miwili nyuma kua naiona United ikiwa imerejea, Na watu wanasema hapana lakini mimi naiona imerejea najua hilo na ninahisi hivo. Namna United wanacheza sasa ni namna ambavyo walikua wanacheza kwenye historia yao”GuardiolaKocha huyo anaamini kua klabu hiyo iliyo chini ya kocha Erik Ten Hag imeimarika kwa kiwango kikubwa sana na imeweza kua shindani kwa kippindi cha hivi karibuni. Swali kubwa ni kua klabu ya Manchester United itaendeleza ubabe wake kushinda mfululizo na kufuta uteja wa kupoteza michezo mitatu mfululizo katika mchezo wa leo.

Acha ujumbe